Ruka hadi maudhui
PrimePath

Fungua milango mipya ya kidijitali kwa taasisi yako.

Teknolojia ya vitendo, kuanzia mkakati hadi mfumo unaofanya kazi, ili ufanye kazi kwa uwazi, ufanisi na kujiamini.

Kikao cha bure cha dakika 45 kuelewa shughuli zako na pale mfumo unapoweza kusaidia.

Kutoka daftari la fedha hadi kukopesheka.

Benki na wawekezaji hufadhili kile wanachoweza kuthibitisha. Biashara inayoendeshwa kwa daftari na kumbukumbu za kichwani haiwezi kuonyesha hilo, hata ikiwa nzuri kiasi gani.

Kumbukumbu sahihi za kidijitali zinabadilisha hilo. Kila mauzo, malipo na mwendo wa stoo unarekodiwa papo hapo, hivyo hesabu zako zinakubaliana, unaona biashara hata ukiwa mbali, na una kumbukumbu ambazo benki inaweza kuziamini. Hicho ndicho kinachofanya biashara ikue, ikopesheke na iwe tayari kwa wawekezaji.

Tazama PrimeTill kwa chini ya dakika tatu
  1. Daftari na kumbukumbu za kichwani
  2. Kumbukumbu safi za kila siku
  3. Inakopesheka na iko tayari kukua

Define, Design, Drive.

Kila mfumo tunaojenga unafuata njia ileile, kuanzia kusoma shughuli zako hadi kuendesha mfumo pamoja nawe.

Mbinu yetu kwa undani (Kiingereza)
A small team in discussion around a laptop at a meeting table
  1. Define

    Tunasoma shughuli zako mahali pa kazi.

    Nani anafanya nini, pesa na taarifa zinapita wapi, na wapi mambo yanaharibika. Unapata picha wazi ya tatizo kabla msimbo wowote haujaandikwa.

  2. Design

    Tunapanga mfumo kulingana na utaratibu wako.

    Skrini, ripoti, idhini, na muunganiko na mifumo ya malipo na ya serikali. Unaidhinisha kabla hatujajenga.

  3. Drive

    Tunajenga, tunazindua, tunafundisha na tunabaki.

    Timu yako inafundishwa kwenye mfumo unaofanya kazi, na tunabaki kusaidia, kuboresha na kuukuza kadiri unavyokua.

Mshirika anayeanza kazini na kubaki baada ya uzinduzi.

Tunajenga kwa ajili ya Tanzania.
Tunaelewa GePG (mfumo wa malipo ya serikali), pesa za simu, matakwa ya TRA (mamlaka ya kodi) na jinsi halmashauri zinavyofanya kazi.
Tunaanza kazini, si kwenye slaidi.
Define inamaanisha tunasoma shughuli zako halisi kabla ya kujenga.
Tunamiliki bidhaa zetu.
PrimeTMS, SafiTrack na PrimeTill zinaonyesha tunajenga mifumo inayodumu.
Tunabaki baada ya uzinduzi.
Drive inamaanisha msaada, mafunzo na maboresho endelevu.
Timu moja, mwanzo hadi mwisho.
Mkakati, usanifu, ujenzi na msaada mahali pamoja.

Mifumo tuliyowasilisha.

Kazi za wateja tunazoweza kutaja hadharani.

  • ASKUNI

    CRM system

    A customer relationship management platform for streamlined client engagement.

  • Rakoli

    Website and MIS

    A corporate website with an integrated management information system (MIS).

Kuwa mshirika anayeaminika zaidi Tanzania katika kujenga mifumo ya kidijitali inayoendesha maendeleo ya taifa.

Tuambie jinsi shughuli zako zinavyoendeshwa leo.

Kikao cha bure cha dakika 45 kuelewa shughuli zako na pale mfumo unapoweza kusaidia.

Njia nyingine za kuwasiliana
Ungependa nini?